Tanzanite yatwaa Kombe la COSAFA U20 Wanawake


Timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Zambia leo Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth.

Mabao ya Tanzania inayofundishwa na kocha Bakari Nyundo Shime anayesaidiwa na Edna Lema yamefungwa na Opa Clement dakika ya 24 na Protasia Mbunde dakika ya 87.

Ushindi huo pia ni sawa na kulipa kisasi kwa Tanzanite baada ya kufungwa mabao 2-1 pia na Zambia katika mchezo wa awali, kwenye Kundi B. Ikumbukwe Tanzania iliingia fainali baada ya kuwafunga wenyeji, Afrika Kusini Uwanja wa Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth.