TPA yakabidhi Mashine mbili kwa ajili ya kuhifadhi watoto Njiti


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa mashine mbili za incubator kwaajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh. milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga.


Akikabidhi msaada huo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Witonde Philipo amesema kuwa mamlaka hiyo ilikuwa imetenga bajeti ya Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia jamii katika sekta ya elimu na afya.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Witonde alisema kwamba wao wanashukuru kupewa nafasi ya kujumuika kwenye mkoa wa Tanga kusaidia kuboresha maisha ya wakazi wa mkoa huo.

Alisema kwamba walipata maombi ya kuwepo kwa changamoto hizo na wao wakaona wafanye jambo hilo hivyo wanaimani uongozi wa mkoa huu ungeweza kupata watu wengine lakini wakawaona wao.

Mhandisi Witonde alisema kwamba mamlaka hiyo imekuwa na utaratibu kila mwaka kutenga bajeti kwa ajili ya kusaidia jamii kwenye ameneo ya afya, elimu na maeneo mengine ya kijamii.

Alisema katika mwaka wa fedha walipanga kutumia kiasi cha milioni 50 kutoa huduma hizo huku akieleza kwamba vifaa hivyo vitasaidia kuokoa maisha ya watoto.

“Kabla ya zoezi hili siku chache tulikwisha kukabidhi mabati 378 shule ya sekondari Tanga School yenye thamani ya milioni 15 na yamekarabati nyumba tano lakini pia tutaendelea kuona namna ya kuwasaidia kwa kadiri mungu atakavyowajalia”Alisema

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwashukuru TPA kwa kutenga fedha hizo milioni 50 kwenye mwaka wa fedha na kuwezesha kwenye katika mkoa wetu kuleta vifaa hvyo ambavyo vitakuwa ni chachu kuwasaidia kuboresha sekta ya afya.
Alisema kwani kutenga fedha ni jambo moja na kufanikisha ni jambo la pili hivyo niwapongeze TPA kwa kutekeleza wale walioyapanga na kuhaidi

“Nimshukuru MKurugenzi Mkuu wa TPA kwani Tanga imekuwa ni nyumbani kwenu kuja mara kwa mara na kuweza kuwasaidia tunatambua jitihada kubwa mnazofanya katika kuhakikisha mnasaidia jamii na watanzania kwa ujumla”Alisema

Alisema wanatambua jitihada kubwa mnazofanya TPA kuhakikisha mnasaidia jamii na watanzania kwa ujumla ukiacha suala la kusimamia mapato na kujenga mazingira mazuri ya kuwa lango kuu la kibiashara kati ya nchi yetu na jirahi bandari imekuwa ni msaada kuwasaidia shughuli mbalimbali za kijamii na maelezo yako ulioyayatoa yanadhihiridha

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa huo, Abdiel Makange, amesema mashine hizo zitaweza kusaidia kuokoa maisha ya watoto njiti ambao wanazaliwa katika hospitali hiyo.

“Hospitali ilikuwa ina mashine mbili tayari, hivyo uwepo wa nyingine za ziada kutawezesha kupunguza changamoto ya vifo kwa watoto hao” amesema.