Tuna vivutio vingi vya utalii na mazao mengi ya biashara - DC Ngara


Na Clavery Christian Bukoba

Mkurugenzi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera amesema kuwa Wilaya ya Ngara ni moja kati ya wilaya za mkoa Kagera zenye vivutio vingi vya utalii na uwekezaji mzuri wa biashara kwasababu wanalima mazao mbalimbali ya biashara na yenye masoko makubwa hapa nchini na nje ya nchi kama vile kahawa na ndizi.

Akizungumza na Muungwana Blog Mkurungenzi wa Wilaya ya Ngara, Bw, Aidan John Bahama amesema kuwa watu wa mkoa wa Kagera na Ngara wanaweza kukuza biashara zao kwa kupitia kongamano la wiki ya Kagera ambapo watapata fursa ya kukutana na wafanyabiashara mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Bw, Aidan Bahama amesema kuwa halmashauri yake imewawezesha vijana kujiajiri kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya asilimia 10% ambapo amesema kuwa tiali matunda yake yameanza kuonekana na wao kama halsmashauri wanaendelea na mpango wa kuwataftia maeneo ya kuja kuwekeza kwa ajiri ya viwanda na watu watakao kuja kuwekeza katika wilaya hiyo wasikwame na kupata shida.

Wilaya ya Ngara inapakana na nchi ya Rwanda na inamaeneo ya ufugaji, kilimo pia ina madini ambayo utumika kutengeneza bati na chuma. Bw,  Bahama amewaomba wawekezaji na wafanya biashara kutoka maeneo mbali mbali hapa nchini kwenda kuwekeza katika wilaya ya Ngara ambapo wataweza kuuza na kununua nje ya nchi bidhaa zao bila wasi wasi na kwa haraka zaidi.

Wilaya ya Ngara imeshiri kikamilifu katika kongamano la wiki ya uwekezaji mkoani Kagera linalofanyika katika viwanja vya gymkhana mjini Bukoba ambapo kongamano hilo litahitimishwa agost 17 mwaka huu.