Uganda: Watu 22 wathibitishwa kufariki katika ajali ya mlipuko wa lori la mafuta


Msemaji wa jeshi la polisi mkoa wa Great Bushenyi nchini Uganda, Marshal Tumusiime amesema, watu zaidi ya 22 wamethibitishwa kufariki katika ajali ya mlipuko wa lori la mafuta katika mtaa wa Rubirizi, magharibi ya nchi hiyo.

Bw. Tumusiime amesema timu ya pamoja ya uokoaji imepata miili 17 ya watu walioungua vibaya ambayo haiwezi kutambuliwa, pamoja na mingine 5 ambayo imetambuliwa kwenye eneo la ajali katika kituo cha biashara kando na Barabara kuu ya Mbarara-Kasese.

Hapo jana Mkuu wa Wilaya ya Rubirizi, Harriet Nabukenya akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo alisema dereva wa lori la mafuta alishindwa kudhibiti mwendo wa lori hilo na kuvamia teksi mbili za abiria zilizokuwa zimeegeshwa barabarani