Umoja wa Ulaya watafuta Dola Milioni 56 kuwasaidia wanaokumbwa na njaa Afrika Mashariki


Umoja wa Ulaya (EU) umesema kwamba unatafuta Dola Milioni 56 kwa ajili ya kusaidia watu wanaokumbwa na njaa katika kanda ya Afrika Mashariki.

Muungano huo umesema kwamba fedha hizo zitatumika kusaidia watu milioni 28 nchini Somalia, watu milioni 22.6 nchini Ethiopia, watu milioni 3 nchini Kenya na watu milioni 2.24 nchini Uganda wote ambao wanakumbwa na kiangazi.

“Katika ziara zangu kwenye nchi za kanda ya Afrika Mashariki nimeshuhudia jinsi mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri wakazi wa eneo hili. Msaada wetu utawezesha waathiriwa kupokea usaidizi wa kibinadamu,” alisema Christos Stylianides- kamishna wa msaada wa kibinadamu na udhibiti wa majanga wa EU.