Loading...

8/16/2019

Van Dijk kuchuana vikali dhidi ya Messi na Ronaldo


Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk atashindania taji la Mwanasoka Bora wa mwaka 2019 barani Ulaya baada ya kuorodheshwa katika wanafainali watatu wa mwisho katika kura zilizopigwa jana.

Mholanzi huyo atawania taji hilo la kifahari dhidi ya wanasoka wengine maarufu Lionel Messi (Barcelona) na Cristiano Ronaldo (Juventus).

 Mreno Ronaldo ni mshindi wa tuzo hii mwaka 2014, 2016 na 2017 naye raia wa Argentina Messi aliibuka mshindi mwaka 2011 na 2015. Van Dijk anaingia kwa mara ya kwanza katika orodha ya kuwania tuzo hiyo iliyoanzishwa mwaka 2011.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger