Na. Ferdinand Shayo, Arusha
Viongozi wa Baraza la wafugaji wilaya ya Ngorongoro wamesimamishwa nafasi zao ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ikiwemo kushindwa kusimamia majukumu ya baraza hilo.
Mwenyekiti mteule wa baraza hilo Lengai Muluo amesema kuwa wamechukua hatua hiyo baada ya kupiga kura ya kutokua na imani na viongozi hao iliyopigwa na wajumbe 56 wa baraza hilo kati ya wajumbe 72
Akizungumza na Wanahabari wamesema kuwa viongozi wamesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja mpaka pale kamati itakapojirisha na masuala ya uendeshaji wa baraza hilo la wafugaji kama hajutakuwepo na ukiukwaji wa katiba ya baraza hilo.
Mjumbe wa Baraza hilo Emanuel Shanghai kuwa kwa sasa kamati hiyo imewaweka viongozi hao pembeni ili waweze kuitisha mkutano mkuu ambao utafanya maamuzi juu ya hatma ya viongozi hao iwapo watakutwa na makosa watawajibishwa.
Mkazi wa Ngorongoro James Moringe amesema kuwa kwa Mara ya kwanza viongozi kusimamishwa tangu kuanzishwa kwa baraza hilo hivyo anaamini busara itatumika ili baraza hilo liendelee kutoma huduma kwa wananchi.
Meneja wa Baraza hilo Peter Metele akiongea kwa njia ya simu amekanusha kuwepo kwa tetesi za kuvuliwa uongozi kwani mpaka sasa hawajapata taarifa rasmi zaidi ya kuona kwenye mitandao.
