Wachezaji wa Raga kutoka Kenya wapatikana na hatia ya kubaka


Wachezaji wa Raga Alex Mahaga Olaba na Lawrence Frank Wanyama jana walipatikana na hatia ya kumbaka mwanamuziki. Mwanamke huyo anawashutumu wachezaji hao wa Harlequin ya Kenya kwa kumbaka usiku wa siku yake ya kuzaliwa February 10, 2018 huko Nairobi.

Baada ya kubakwa alipata ujauzito na baadaye wabakaji wakamtishia kumshtaki endapo ataamua kutangaza suala hilo.

Olaba na Wanyama watahukumiwa leo Ijumaa. Mwezi uliopita jaji Martha Mutuku alitoa kibali cha kukamatwa kwa Mahaga kufuatia ombi la upande wa mashtaka baada ya kutofika mahakamani kwa mara ya pili.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items