Walanguzi wanavyowakandamiza wakulima wa Parachichi Njombe



Na Amiri kilagalila-Njombe

Kuruhusiwa kwa soko huria nchini kumetajwa Kuwa ni moja ya changamoto inayowakumba  wakulima wa zao la matunda ya parachichi wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe  na kusababisha kushindwa kuuza matunda wanayoyazalisha shambani kwa faida kutokana na kuibuka kwa bei tofauti tofauti katika wilaya hiyo.


Baadhi ya wakulima wa zao la matunda aina ya parachichi wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wamekutana katika kijiji cha Mlevela na kufanya mkutano wa kujadili changamoto za ukosefu wa masoko pamoja na  namna wanavyoshindwa kunufaika na kilimo hicho na badala yake kujikuta wakilanguliwa na wanunuzi wa matunda hayo.

Natolina Mzavala na Christopher Mgaya wanasema hali hiyo imekuwa kikwazo kwao kwa sasa huku wakihitaji kuundwa kwa ushirika wa pamoja ili kuwa na sauti ya pamoja.

“Tukiwa na ushirika tutakuwa na sauti ya pamoja amabyo itatuwezesha kupata wanunuzi wa aina moja,na watu hapa ni mashahidi kuna watu bado tunayo matunda kwenye miti sijui tunaweza kufanyaje ili tupate kuuza”aliseama Natolia mzavala mmoja wa wakulima.

Jaires Mhema ni mwenyekiti wa mtandao wa parachichi wilayani Waging'ombe mkoani Njombe Anaeleza kuwa walanguzi wamekuwa wakiwakandamiza zaidi wakulima kwa sasa.

“Walanguzi huwa wanakuja kila mmoja na bei yake,mnaweza mkajadili bei ya pamoja ambayo mwaka huu tulijadili shilingi 1500,lakini matokeo zinakuja kampuni zinapitia kwa madalali zinachukua kwa shilingi 1200 au 1300,kuna kampuni moja imekuja na hao ndio wameshuka sana wamechukua hasi liject kwa shilingi 300”alisema Jaires Mhema.

Mwenyekiti wa mtandao wa parachichi mkoa wa Njombe Frank Mgaya amesema uzalishaji wa matunda ya parachichi yaliyo na tija kwenye soko la dunia umekuwa ni duni na hivyo asilimia 50 ya matunda yanakosa sifa ya kuuzwa kwenye soko la kimataifa.

“Shida kubwa ya Njombe ni ubora wa mazao yetu unakuta yanayouzwa kwenda nje ni asilimia 50 na asilimia 50 nyingine yanabaki hapa ndani kwasababu yanakosa sifa”alisema Mgaya
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items