Waliokuwa wafanyakazi wa Airtel Kenya waibuka na mapya Mahakamani


Waliokuwa wafanya kazi wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel nchini Kenya wamepinga mpango wa kuunganisha kampuni hiyo na ile ya Telkom Kenya wakisema kwanza wanataka walipwe fidia ya dola milioni 1.

Kupitia ilani waliotoa kwa mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya, wafanyakazi hao wanasema itakuwa vigumu kwao kupata fidia yao baada ya kuungwanishwa kwa kampuni hizo.

Kwenye kesi waliowasilisha katika mahakamani kupitia kwa wakili wao Duncan Okatch wafanyakazi hao 52 wanasema walifutwa kazi kimakosa mwaka 2016.

Airtel ilisema Februari kuwa ilikubaliana na Telkom Kenya kuwa kitu kimoja ili kuongeza mgao wake wa soko la kushindana kikamilifu na Safaricom ambayo ina mgao wa asilimia 65.