Wananchi kushiriki miradi ya elimu kwaboresha miundo mbinu na taaluma Momba




Na, Baraka Messa, Songwe.

Wananchi kushiriki katika ujenzi wa miradi ya elimu kwaimarisha na kuboresha miundo mbinu mashuleni na kuimalika kwa taaluma katika  halmashauri ya  wilayani Momba mkoani Songwe .

hayo yamebainika katika ziara ya kamati ya Siasa mkoani chama cha Mapinduzi mkoani  Songwe ambapo ushiriki mzuri wa wananchi katika miradi ya elimu imeonekana kujenga miundo mbinu mizuri iliyo kamilika kwa wakati tofauti na maeneo mengine mkoani humo.

 Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Songwe Elniko Mkolla alizitaka halmashauri nyingine za mkoa wa Songwe kujifunza kutoka halmashauri ya Momba namna wananchi walivoshiriki katika kujitolea nguvu zao na michango mbalimbali kufanikisha kutatua uhaba wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo pamoja na mabweni kwa baadhi za shule.

"nimefurahishwa sana na namna wananchi wa Momba na viongozi namna walivyoshirikiana katika zoezi hili la ujenzi wa miundo mbinu katika shule za serikali, majengo yamejengwa vizuri kwa hili viongozi pamoja na wanchi mnastahili pongezi, ningependa madarasa haya kutokana na uimara wake na kukidhi vigezo yawe madarasa ya mfano kwa halmashauri zingine kuja kujifunza" alisema mkolla.

Pia Mkolla aliwataka wananchi kushiriki kuitunza kuitunza  vema miradi hiyo mizuri ambayo ni utekelezaji wa irani ya chama cha Mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuimalisha sekta ya Elimu kuanzia elimu ya awali mpaka Sekondari.

"Rais anahangaika sana kutafuta hizi pesa za miradi mbalimbali hivyo ninyi viongozi msamie miradi hii tukishirikiana na wananchi yatupasa kuisimamia vema na kuhakikisha tunaitumia vizuri ikiwa ni pamoja na kufaurisha wanafunzi wengi kwenda Sekondari ili kujenga Taifa imara lenye watalaam mbalimbali" aliongeza Mkolla.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Songwe Brigedia Nicodemas Mwangela akiambatana na kamati ya Siasa mkoa aliwata viongozi na wasimamizi kuthaminisha nguvu za wananchi kwa kila miradi ili kujua wa michango yao ni kiasi gani katika katika miradi wanayo shiriki.

aidha mkuu wa mkoa aliwataka wananchi kuendelea kushiriki katika miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa , matundu ya vyoo pamoja ujenzi wa mabweni kutokana na ongezeko la wanafunzi ambalo huongezeka kila mwaka.

"Hii miradi ni endelevu hivyo wananchi msichoke kuendelea kujitoa kataika shughuli mbalimbali za maendeleo katika shule zetu kuanzia msingi mpaka Sekondari hii itasaidia kuimalisha elimu yetu" alisema Mwangela Mkuu wa mkoa.

Jeofrey Mwampas afisa Mipango Momba alisema ushirikiano mzuri wa watalaam, viongozi wa kata ambao  ni madiwani, wananchi pamoja na viongozi wa Halmashauri ndio siri kubwa ya kusimamia na kujenga miundo mbinu bora ya elimu na kuimalika kwa taaluma katika shule za Msingi katika Halmashauri hiyo.

Alisema ushirikiano huo ulipelekea kuwa na uwazi katika fedha zilizotengwa kawa ajili ya miradi hiyo muhimu na kuunda kamati ambazo zinashirikisha wananchi huku walimu wakuu wakiwa wasimamizi wakubwa katika ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo na mabweni.

Gaudence Assey afisa elimu msingi katika halmashaur ya Momba alisema kuwa pamoja na madarasa mengi yaliyojengwa Halmashauri hiyo bado inakumbwa na upungufu wa walimu  pamoja na madarasa hali ambayo hupelekea walimu kuwakusanya wanafunzi katika darasa moja wakati wa kufundisha.