Watumishi watakao kwamisha uwekezaji waonywa


Na Clavery Christian Bukoba

Naibu Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Stella Manyanya amewaonya Watumishi wa serikali watakao kwamisha shughuli ya uwekezaji na kusababisha azimio la wiki ya uwekezaji Mkoani Kagera kushindwa kufikia malengo yake yaliyokusudiwa.


Amesema kuwa ni wakati sasa wa kila mmoja kuwa tiali kupokea uwekezaji katika mkoa Kagra ili iwe raisi kukuza uchumi wa mwananchi mmoj mmoja wa mkoa kagera na taifa kwa ujumla.

Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa mkoa Kagera ni moja ya Mikoa mitano Tanzania yenye fursanyingi za uwekezaji na ndiyo mikoa inayoongoza kwa kuwa na chakula cha kutosha ila inakabiliwa na ukosefu wa lishe kwa wakazi wake.

Manyanya amesema kuwa fursa za biashara ni nyingi ila hazijatumika vizri ndani ya mkoa kagera ambapo amewataka wafanyabiashara kuzingatia ubora wa bidhaa zao ambapo amesema kuwa kuwekeza katika mkoa Kagera kuna faida nyingi ambapo utapata masoko ya nchi mbalimbali za Afrika na dunia kwa ujumla.

Akihutubia wafanya biashara na viongozi mbalimbali walioudhuria katika kufunga kongamano la wiki ya uwekezaji mkoani Kagera amesema mada zote walizowasilisha zimezingatia fursa za uwekezaji mkoan Kagera aidha amesema kuwa Kagera kuna mazingira rafiki ya uwekezaji ndani ya mkoa Kagera.

Waziri Manyanya amesema kuwa wizara yake kwa kushirikiana ofisi ya wzri mkuu watakuwa bega kwa bega na wafanyabiashara wote watakaojitokeza kuwekeza mkoani Kagera katika maeneo mbalimbali.

Amesema kupitia Tanzania Kagera inaenda kufanya biashara mpka Africa kusini ambapo amesema kuwa wanaendelea kufanya mawazungumzo katika mkutano wa SADEC ili lugha ya kiswahili iweze kuwa lugha rasmi ya nchi za SADEC Afrika.

Manyanya amewataka watanzania kuacha tabia isiyo nzuri ya kuikashifu nchi ya ya Tanzania eti mazingira ya tanzania siyo mazuri kuwekeza.