Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepokea msaada wa Pikipiki ambazo zitatumika kwa ajili ya doria ili kupunguza uhalifu Mkoa wa Iringa.
Aidha, amelitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kutotumia Pikipiki hizo kwa ajili ya kazi za kihalifu ikiwemo kusingikiza mirungi na badala yake zitumike kwa kazi iliyokusudiwa.
Lugola alitoa kauli hiyo, wakati akipokea msaada wa Pikipiki mbili zenye thamani ya Tsh 2.8 zilizotolewa na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto kwa ajili ya kituo cha Ikokoto Iringa.
“Tumepokea Pikipiki hizi, wazitunze ili zidumu zitumike kwaajili ya kufanya doria kwenye maeneo korofi hususani maeneo ya mlima Kitonga,”alisisitiza.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi na wadau werevu kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi kamwe wasichoke kutoa misaada kwa Jeshi la polisi.
