Waziri Lukuvi aendelea na utatuzi wa migogoro ya ardhi


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameendelea na utatuzi wa migogoro ya ardhi ambapo sasa amekutana na Watawa wa Holy Spirit Sisters kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro wa shamba la Kilari lililopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

Katika mgogoro huo jumla ya ekari 284 kati ya ekari 1410 zinazomilikiwa na Masisters zimevamiwa na ndani ya shamba lililovamiwa lina kaya 254 zenye idadi ya watu 1283.

Kikao kati ya Lukuvi na Masisters ni muendelezo wa vikao vya kutafuta namna bora ya kutekeleza amri ya Mahakama iliyowapa ushindi Masisters dhidi ya wavamizi.

Mpya zaidi Nzee zaidi