Waziri wa Elimu ashiriki mkutano CAPA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameshiriki mkutano wa Umoja wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Ufundi wa Nchi za Afrika Wanachama Jumuiya ya Madola (Commonwealth Association of Technical Universities and Polytechnics in Africa -CAPA) nchini Rwanda.

Mkutano huo ambao umeipa Tanzania fursa ya kushiriki katika majadiliano ya namna ya kubadilisha mtazamo juu ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) wa kuifanya elimu hiyo kuwa kiungo muhimu katika kuleta maendeleo ya Viwanda Afrika.

Aidha, mkutano huo umejadili namna ya kuboresha mafunzo ya ufundi na kukuza ubunifu na ujasiriamali kwa vijana ili kuwezesha kuzalisha ajira na fursa za kiuchumi.

Tanzania ni Mwanachama wa CAPA na Taasisi mbalimbali za elimu ya ufundi na elimu ya juu zinashiriki katika shughuli za ushirikiano. Taasisi hizo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Mpya zaidi Nzee zaidi