https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wizara ya Afya yamtembelea mbunifu wa teknolojia ya kusafisha maji | Muungwana BLOG

Wizara ya Afya yamtembelea mbunifu wa teknolojia ya kusafisha maji


Viongozi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi wamemtembelea mbunifu wa teknolojia ya kusafisha maji ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela kilichoko Arusha Dkt. Askwar Hilonga.

Katika ziara hiyo Dkt. Hilonga amewaonesha viongozi hao Teknolojia iitwao Nano Filter yenye uwezo wa kusafisha maji, kuondoa bacteria na virusi, huondoa fluoride na madini yote ambayo hayatakiwi kwa binadamu na kuyafanya maji kuwa safi na salama kwa watumiaji na kwa gharama nafuu zaidi.

Dkt. Hilonga ana tuzo 17 kutoka taasisi na mashirika mbalimbali kutokana na ubunifu huo huku tuzo yake kubwa ikiwa ni ile aliyoipata kwenye kikao cha dunia cha masuala ya afya (World Health Assembly) kilichofanyika Jijini Geneva, Uswisi mwezi Mei mwaka huu.