https://monetag.com/?ref_id=TTIb Adakwa na Madini ya Tanzanite, alikuwa kayaficha sehemu nyeti | Muungwana BLOG

Adakwa na Madini ya Tanzanite, alikuwa kayaficha sehemu nyeti



Na John Walter-Manyara

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amesema wamefanikiwa kuwakamata watu wawili waliokuwa wakijaribu kutorosha madini aina ya Tanzanite kupitia kwenye Ukuta wa Magufuli Mirerani wilayani Simanjiro.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda Senga amesema tangu ukuta wa Magufuli ukamilike,utoroshaji wa madini ya Tanzanite umepungua kwa kiasi kikubwa na jeshi la polisi mkoani hapo limeimarisha Ulinzi ili kuhakikisha hakuna wizi wowote katika machimbo hayo.

Amewataja waliokamatwa ni Issaya Silvanus (UKUKU) 43 Mkazi wa kijiji cha Songambele Mirerani akiwa ameyaficha sehem zake za siri yenye thamani ya shilingi laki 368,310.05 gramu 17 gerdi ya chini huku mtuhumiwa mwingine ambaye ni Yohana Alais (Laiza) 40 mkazi wa kijiji cha Kilima hewa Mirerani yenye thamani ya shilingi Milioni 4,549,698.85 sawa na gramu 17 gredi ya juu.

Aidha Kamanda amewatahadharisha wenye nia ovu ya kuhujumu Uchumi wa nchi kwa kutorosha Madini kwa kuwaeleza kuwa mwanya huo haupo tena na haiwezekani katika mkoa wa Manyara.