Wananchi Njombe mjini walia na gharama za maji



Na Amiri kilagalila –Njombe

Baadhi ya wakazi wa mji wa Njombe akiwemo Maria Haule na Restita Msemwa wameitupia lawama mamlaka ya maji Njombe mjini NJUWASA kwa kuwa na mgao kipindi chote cha mwaka pamoja na ongezeko la zaidi ya asilimia 50 ya tozo za maji hali ambayo inawafanya baadhi yao kuamua kuchota mabondeni.

Wakizungumza na MUUNGWANA BLOG baadhi ya wakazi wa mitaa ya mji wa Njombe wamesema hali ya upatikanaji wa maji  imeendelea kuwa ngumu huku wengine wakilalamika juu ya tozo za maji ambazo zimekuwa zikipandishwa mara kwa mara.


“Yaani bili ingepungua tunateseka kweli kweli maana inatoka elfu 30,25 lakini maji hayatoki,mda mwingine tunawaza hivi ni kwanini bila inapanda sana”alisema Maria Haule mkazi wa Posta kati

Akitolea ufafanuzi sababu ya kuongezwa kwa tozo za maji mkurugenzi wa mamlaka ya maji Njombe mjini NJUWASA mhandisi John Mtyauli anasema mamlaka imelazimika kufanya hivyo ili kupata fedha na mradi uweze kujiendesha

“Utaratibu wa zamani na sasa katika malaka zetu upo tofauti,hapo awali serikali ilikuwa inasapoti ikiwemo ghalama za umeme, lakini kwa sasa yapo majukumu ambayo yameainishwa wazi kwamba hakutakuwa na msaada wowote kutoka wizara ya maji hivyo mamlaka yenyewe iweze kusimama kuhakikisha huduma inakuwa endelevu,kwa hiyo ili kuufanya mradi ambao serikali imewekeza uweze kufanya kazi hiyo ni moja ya sababu iliyofanya kuwe na ongezeko la bili za maji”alisema Mtyauli

Aidha amesema halmashauri ya mji wa Njombe ipo mbioni kumaliza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji bomba, baada ya serikali kukamilisha usanifu wa ujenzi wa mradi mkubwa wa maji katika mto hagafilo wenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita mil 17 kwa siku.

Hata hivyo amesema kwasasa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Njombe NJUWASA ina uwezo mdogo ambapo inatajwa kuzalisha lita mil 3 pekee kwa siku, wakati mahitaji ya mji yakiwa ni lita mil 12 jambo ambalo limeilazimu mamlaka hiyo kufanya mgao wa huduma hiyo ili kila mtaa uweze kuipata huduma hiyo.

“Hivi sasa tuna mradi mkubwa ambao tunategemea utaanza ikimpendeza Mungu tunategemea mwezi wa 12 unaweza ukaanza,na mpaka sasa mhandisi mshauri ameshapatikana na jukumu hili linasimamiwa na wizara kwa kushirikiana na wataalamu wa Njuwasa mhandisi mshauri alishalipoti tangu mwezi wa nane ikiwa ni ahadi ya waziri katika ziara ya Mh Rais,na mpaka sasa wameshafanya kazi kadhaa ikiwemo upimaji na usanifu”aliongeza Mtyauli

Awali tozo za maji ilikuwa ni shilingi 900 kiwango cha chini huku cha juu kikiwa ni 1100 , wakati bei mpya kiwango cha chini kikiwa shiling 1449 huku cha juu kikiwa 1632.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items