Na Edina Fidelis, Morogoro.
Kufuatia ajali ya moto iliyotokea eneo la Msamvu manispaa ya Morogoro baada ya lori lililokuwa limebeba mafuta kulipuka na kusabisha vifo vya watu Zaidi ya mia moja, banki ya posta hapa nchini [TpB] imekabidhi vifaa tiba kwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro vyenye thamani ya shilingi milioni tatu laki tisa sabini na sita na mia tano kwa ajili ya majeruhi wa ajali hiyo ambao bado wanaendelea na matibabu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba kwa mkuu wa wilaya ya Morogoro meneja wa banki ya posta [TpB] Eliwangu Mwangama alieleza kuwa kama banki imeona ipo haja ya kutoa faida kama fungu kwa ajili ya kusaidia jamii hususani kwa upande wa afya na kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia kutoa huduma kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto na kufidia vifaa vilivyotumika.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo alieleza kuwa vifaa tiba vilivyotolewa vitaimalisha kitengo cha dharula cha ICU na kuwaomba wadau mbalimbali kuweza kujitolea kwani uhitaji bado ni mkubwa wa kujiweka utayari kwa ajili ya kuimalisha huduma za kiafya katika kitengo cha maafa kutokana na Mkoa huo kuwa katikati ya mikoa mingine.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro Dkt. Rita Lyamuya alieleza kuwa kulikuwa na wagonjwa wa ajali ya moto ambao walikuwa kumi na nane wakipatiwa matibabu na hali zao wanaendelea kutengemaa na kurusiwa kurudi nyumbani na kwa sasa wamebaki wanne wakiendelea na matibabu na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kutoa misada mbalimbali ili kuimalisha huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo huku mganga mkuu mkoa wa Morogoro Dkt.AR Kusirye Ukio alieleza kuwa vifaa tiba vitasaidia kutoa huduma kama ilivyokusudiwa na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kwani uwitaji bado mkubwa.