Ajali ya Gari yaua Saba na kujeruhi wengine 18 Mkoani Manyara


Na John Walter, Simanjiro-Manyara.

Watu saba  wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea kijiji cha Namalulu kata ya Naberera wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Augustino Senga alisema tukio hilo lilitokea Septemba 09 mwaka huu majira ya saa 07:00 jioni huko wilayani Simanjiro.

Kamanda Senga amesema Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa fuso aina ya Mitsubish T. 870 AHG kushindwa kulimudu  kutokana na kona nyingi na milima katika eneo la Namalulu hali iyopelekea gari  lililokuwa linatokea Arusha kwenda Simanjiro kuingia korongoni na kupinduka.

Kamanda Senga aliwataja marehemu hao kuwa ni Leapa Olekaraa (31), Aloyce Temba (32) mkazi wa Arusha, Moses Mgonja (31) mkazi wa Rombo Kilimanjaro, Germana Gerard (36) mkazi wa Arusha na Anna Kileo (46) mkazi wa Sanya juu Kilimanjaro.

Hata hivyo Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Zahanati ya Orkesment lakini mpaka asubuhi ya leo waliokwisha kutambuliwa na ndugu zao ni miili mitatu na miili miwili bado haijatambuliwa.