AliKiba ajibu ishu ya kuachana na Mke wake


Baada ya kuenea katika mitandao ya kijamii Msanii wa Muziki AliKiba kuachana na Mke wake, Amina Kesh. AliKiba ameibuka kujibu tuhuma hizo.

AliKiba amesema kuwa “Ni kweli mimi na mke wangu tuna migogoro na ni jambo la kawaida kwenye ndoa, ila sijampa talaka hata moja.”

“Kwa sasa mke wangu yupo nyumbani kwetu kwingine Mombasa, nilimrudisha kule kwa muda wakati nilipoenda on Europe Tour, pia Amina ni msomi, kukaa tu ndani nilikuwa simtendei haki, nikaona bora arudi kazini.”

“Taarifa za kwamba mke wangu hapendi ndugu zangu si za kweli, maisha yangu anayajua coz nimeishi nae kwa muda wa miaka 3 kabla ya ndoa. Sijapendezwa kabisa na watu wanaosema mke wangu mshirikina. Yote ya uongo.”