Azam FC yatangulia Zmbabwe bila kocha mkuu

Kikosi cha Azam FC leo kimekwea pipa kuelekea Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Triangle United.

Msafara wa leo umeongozwa na Kocha Msaidizi Idd Cheche akiwa na baadhi ya wachezaji ambao hawakuitwa timu ya Taifa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 28 katika jiji la Bulawayo.

Mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Azam ilikubali kichapo cha bao 1-0 ili isonge mbele ni lazima ishinde mchezo wa marudio kwa mabao zaidi ya mawili.