Loading...

9/14/2019

Davido amvisha pete ya uchumba mpenzi wake


Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido ambae anaelekea kuachana na kambi ya ukapera baada ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake Chioma, hatimae ameweka wazi juu ya ujauzito wa mchumba wake huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Davido ameweka wazi jambo hilo, ambapo huyu atakuwa mtoto wake wa tatu, ikiwa tayari ana mabinti wawili toka kwa wanawake tofauti, Aurora Imade Adeleke pamoja na Hailey Veronica Adeleke.

Davido na Chioma wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu na sasa wameamua kuupeleka uhusiano huo katika hatua nyingine na taarifa zilizopo ni kwamba wanatarajia kufunga ndoa mwakani nchini Nigeria.

Itakumbukwa, kabla kuvishana pete wiki chache zilizopita, Davido na Chioma walikuwa na hafla ya kuzikutanisha familia zao kwa ajili ya utambulisho.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger