Ligi Kuu Soka Zanzibar yaanza kwa kishindo


Na Thabit Madai, Zanzibar

Ligi Kuu soka Zanzibar imeanza rasmi jana kutimua vumbi kwa chezo 3, Unguja 2 na Pemba Mchezo 1.

Katika michezo hiyo Unguja kulipigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ya Jang’ombe boys ilikutana na timu ya KMKM,huku uwanja wa Moa Zedng kulipigwa mchezo kati ya Zimamoto na Jamuhuri ambapo kisiwani Pemba  kulipigwa mchezo kati ya Jku na Mwenge.

Mchezo uliopigwa Mao Zedong timu ya  Zimamoto iliondoka na ushindi baada ya kuicha mabao 5-0 timu ya Jamuhuri mabao yaliofungwa Hassan Haj daika ya 20  na bao la pili Amour Haji dakika ya 39,huku bao la tatu liliongezwa na Ibrahim Hamad Hilika dakika ya 54 bao a nne lilifungwa na Ali Juma dakika ya 56 na bao la tano lilifungwa Hamour Haji dakika ya 62.

Hadi timu hizo zinaondoka uwanjni Zimamoto ilijikuta ikiondoka na mabao matano mkoni mwao.

Mchezo uliopigwa uwanja Gombani Pemba JKU ilitoakichapo  cha mabao 2- dhidi ya Selem mvie  ambayo yalifungwa na Victor Patrik dakika ya 20 na dakika ya sitaipata.

Hadi muamuzi wa mchezo huo anapuliza pyenga yake timu ya JKU iliondoka na pointi tatu,huku Selem mview hakupata kitu.

Mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan timu ya KMKM  ilitoa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Jang’ombe bao ambalo lilifungwa na Ventiraus John dakika ya 82 na kudumu hadi mwisho wa mchezo huo.

Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa kupigwa  michezo miwili,kisiwani Unguja uwanjaMao Zedong timu ya Kipanga na KVZ,huku uwanja wa Gombani timu ya Mafunzo itakutana na timu ya Mwenge ambazo zitapigwa majira ya saa 10 jioni.

Katika michi hizo jopu la makocha lilimchagua Ali Jecha kuwa mchezaji bora ambae alijipatia zawadi ya kiatu cha soka wakati huo huo mchezaji wa KMKM Khaji Mwinyi alijichukulia kadi nyendu baada ya kufanya kosa uwanjani hapo.