JKT kuendelea kufundisha maadili mema na uzalendo kwa vijana




Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Katika kuhakikisha tamaduni za kigeni hazisababishi athari hasi kwa vijana nchini. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limehaidi kuendelea na mkakati wakuwaka pamoja ili kuwajengea uzalendo.

Hayo yalielezwa jana na Kanali Hassan Mabena wakati waufungaji wa mafunzo ya vijana waliohitimu mafunzo ya jeshi kwa mujibu wa sheria katika Kikosi cha Jeshi namba 843 ( KJ 843) kilichopo wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Kanali Mabena ambae katika tukio hilo la ufungaji mafunzo alimwakilisha mkuu wa JKT,  alisema ka
 tika zama hizi za sayansi na teknolojia  kuna muingiliano wa tamaduni zakigeni na zetu. Ambazo baadhi ya tamaduni hizo zinanafasi ya kuharibu mwenendo na tabia za vijana. Ikiwamo kukosa uzaleno kwa nchi na uadilifu.

 '' Katika kipindi hiki cha teknolojia ni muhimu sana kuwajenga  vijana kimalezi. Kwani baadhi ya tamaduni za kigeni haziendani na tamaduni zetu. Kwahiyo kunaumuhimu mkubwa wakuweka pamoja ili wazitambue tamaduni zetu na kuwajengea uzalendo,'' alibainisha Kanali Mabena.

Kwakuzingatia hayo, kamanda Mabena alisema JKT linaendelea kutekeleza mkakati  wa kuongeza vijana katika makambi yake.

Huku likiendelea kuboresha mazingira ya makambi hayo. Ikiwemo kutengeneza na kukarabati miundombinu mbalimbali.

Mabena aliwataka wahitimu hao 1002 washiri kujenga na kukuza uchumi wa nchi kwa kufanyakazi kwa bidii na nidhamu kwa vitendo.

Kwaupande wao wahitimu hao licha ya kuipongeza serikali kurejesha utaratibu wa kupata mafunzo kwa mujibu wa sheria, lakini waliiomba serikali kuongeza muda wa mafunzo.

Katika risala yao iliyosomwa na mhitimu, Catherine Parsalau walisema muda wa mafunzo ni mfupi wakati mafunzo yanayotolewa yanaumuhimu mkubwa.

Kwahiyo serikali aingalie uwezekano wa kurefusha muda wa mafunzo hayo kutoka miezi mitatu na kuwa sita au mwaka mmoja.