Jurgen Klopp azungumzia tabia ya Mo Salah kuwa mchoyo wa pasi


Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema  kuwa tabia ya mchezaji kushindwa kutoa pasi kwa
mchezaji mwingine ni ngumu kuitolea maamuzi hasa  ukizingatia kila mmoja anatimiza wajibu wake ndani ya  uwanja.

Klopp amesema kuwa kitendo ambacho alikifanya  nyota wake Mohamed Salah kwa kushindwa kutoa pasi  kwa Sadio Mane kilikuwa nje ya uwezo wake kwani  kuna wakati mwingine Salah alikuwa akishindwa kutoa  pasi na alifunga mabao yaliyoipa ushindi timu.

Ikumbuke August 31 mwaka kwenye mchezo kati ya Liverpool na Burnley Salah alishindwa kutoa pasi kwa Mane ambaye  alikasirika na kulaumu kitendo hicho licha ya timu yake kushinda kwa mabao 3-0 mchezo wa Ligi Kuu England.