Kauli ya Ed Woodward yamkera Ole Gunnar Solkjaer

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solkjaer ameoneshwa kukerwa na  kauli ya afisa mtendaji mkuu wa timu hiyo  Ed Woodward kwa wawekezaji kuwa ameamua kumpa muda kocha huyo, kauli hiyo Solskjaer anaamini haikuwa inahitajika kwa  Ed Woodward kuwaambiwa wawekezaji.

Kauli ya  Ed Woodward ilitokana kufuatia kuzuka kwa hatma ya Ole Gunnar Solskjaer kuonekana Man United ikipoteza 2-0 dhidi ya West Ham United, Ole Gunnar Solskjaer ameshinda michezo minne 4 kati ya 14 ya Ligi Kuu England toka apewe kibarua cha kudumu mwezi March.

“Ni muhimu kwa sasa tunaendelea kumvumilia Solskjaer akiwa anaendelea kujenga timu yake” Ed Woodward baada ya Solskjaer kuulizwa hilo alijibu tu “Sidhani kama hilo (kuwa wamempa muda)ilikuwa inahitajika” - Solskjaer

Hata hivyo usiku huu Man United itakuwa Old Trafford kucheza dhidi ya Arsenal katika mchezo wao wa 231 toka waanze kukutana, Arsenal akishinda mara 83, sare 48 na Man United ameshinda mara 99, mchezo wa mwisho kati yao walicheza March 10 2o19 na Arsenal ikishinda 2-0.