Kevin Prince Boateng akiri kufanya ujinga uliopindukia


Nyota wa kimataifa wa Ghana anayekipiga katika klabu ya Fiorentina ya nchini Italia Kevin-Prince Boateng amekiri hadharani kuwa alikuwa mjinga wakati akicheza Tottenham Hotspurs ya nchini England (2007-2009).

Boateng ,32, ambaye baada ya miaka miwili Spurs alienda kwa mkopo Borussia Dortmund ameweka wazi kuwa alikuwa akiamini anaweza kuwa na furaha kwa kumiliki na kununua vitu vya thamani (material things) na kujikuta akiishia kucheza mechi 14 na kushindwa kumudu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

"Ulikuwa ni ujinga na niliishi kama mfalme sikuchukulia mchezo wa mpira wa miguu kama kazi nilikuwa mjinga, nilikuwa na kipaji lakini nilikuwa nikifanya mazoezi ya chini ya kiwango kwa saa moja tu uwanjani. Sikuwahi kwenda gym”

"Nilikuwa ndio mtu wa mwisho kufika mazoezini na mtu wa kwanza kuondoka, natoka out na marafiki, nilikuwa na pesa na ninaishi kama mfalme, nilinunua gari tatu ndani ya siku moja nilipokuwa Tottenham Lamboghini, Hummer na Cadillac. Kwa vijana wa sasa ninawaambia huwezi kununua furaha.” Boateng aliongea katika mahojiano na La Repubblica

Ameendelea kwa kusema, "Sikucheza nilikuwa na matatizo ya kifamilia na nikawa nje ya kikosi nikaanza kutafuta furaha kwa kumiliki vitu (material things), sasa gari linakupa furaha kwa wiki . Nilinunua gari tatu ili kuwa na furaha kwa wiki tatu"

Mwaka 2012 iliwahi kuelezwa kuwa mchezaji huyo alikuwa anaandamwa na majeraha kutokana na kufanya mapenzi sana. Mkewe Melissa Satta aliwahi kuripotiwa akisema “ Boateng anakuwa majeruhi mara kwa mara kwa sababu tunafanya mapenzi mara saba mpaka kumi kwa wiki”


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items