Loading...

9/11/2019

Mahujaji 31 wa Shiite wafariki na wengine 100 kujeruhiwa kwa kukanyagana msikitini


Mahujaji 31 wa Shiite wamefariki na wengine 100 kujeruhiwa kutokana na mkanyagano msikitini wakati wa ibada ya Ashura mjini Karbala, kilomita 110 kutoka Baghdad.

Kisa hicho kilitokea masaa ya alasiri, maelfu ya mahujaji kutoka mikoa mbali mbali ya Iraq walipofika kuhudhuria ibada ya Ashura na kuanza msukumano katika lango la msikiti wa Imam Hussein kutokana na idadi yao kubwa .

Mahujaji wa Shiite uadhimisha ibada ya Ashura, kumkumbuka Imam Hussein, mjukuu wa Nabii Mohammed, ambaye aliuawa na kuzikwa mnamo 680 A.D. huko Karbala.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger