Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amepata pigo jingine leo baada ya mwanachama wake mwengine kujiunga na upinzani kwa lengo la kuzuia mpango wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, Brexit.
Waziri wa zamani wa vyuo vikuu Sam Gymah, alitangazwa kuwa mwanachama mpya wa chama cha Liberal Democrat, katika mkutano mkuu wa kila mwaka wa chama hicho mjini Bournemouth kusini mwa pwani ya England.
Gymah ni miongoni mwa wale waliofukuzwa chamani na Boris Johnson ambao wamekuwa wakipaza sauti zao kutaka kura mpya ya maoni ifanyike kuhusu Brexit, na mkosoaji mkubwa wa mpango wa Johnson wa kutaka kuiondoa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31, hata bila ya makubaliano.