Mjane wa rais wa zamani wa Tunisia Beji Caid Essebsi amefariki dunia wakati ambapo nchi hiyo inafanya uchaguzi kumteua Rais mpya baada ya kifo cha mume wake Julai mwaka huu.
Bi. Chadlia Saida Essebsi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83 na kuacha watoto wanne.
Mwishoni Julai, Chadlia alipokea viongozi kadhaa wa kimataifa waliokwenda kumpa pole baada ya kifo cha mumewe.
