Huyu ndio Mtanzania wa kwanza kucheza mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya

Mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya yanaanza leo na safari hii Mtanzania Mbwana Samatta akiwa mmojawapo ya wachezaji watakaoshiriki mashindano hayo akiwa na klabu yake ya Genk.

Genk itashuka dimbani ikiwa ugenini kukipiga na klabu ya Salzburg katika kundi E linalojumuisha vilabu vya Napoli na Liverpool.

Hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Tanzania kuwa na mchezaji anayeshiriki mashindano haya makubwa Ulaya kwa ngazi ya vilabu.