Mwili wa Mugabe wahifadhiwa eneo alilozaliwa, kuzikwa baada ya mwezi mmoja


Mwili wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe umehifadhiwa eneo alilozaliwa mara baada ya watu kumuaga mjini Harare.

Mugabe atazikwa katika makaburi ya mashujaa mjini Harare baada ya mwezi mmoja, kaburi lake litakapomalizika kujengwa.

Awali mipango ya mazishi hayo kufanyika siku ya Jumapili ilifutiliwa mbali. Mugabe ambaye alikuwa na umri wa miaka 95 alifariki wiki iliyopita akipokea matibabu nchini Singapore.
Mpya zaidi Nzee zaidi