Na. Timothy Itembe
Waandishi wametakiwa kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya Kijinsia katika vyombo vya habari hasa kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa Wanawake na Vijana katika uongozi.
Akiongea Beatrice Ezekiel ambaye ni mwezeshaji katika washa ya waandishi wa habari kutoka nje ya Dar es salam juu ya ushiri wa Wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa alisema kuwa kuna haja waandishi kuripoti maswala ya kijinsia katika vyomvo vya habari hasa kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa wanawawake na vijana katika uongozi.
"Kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti maswala kijinsia katika vyombo vya habari hasa kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa Wanawake na Vijana katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi"alisema Ezekiel..
Kwa upande wake mkurugezi wa shirika lisilo la kiserikali TGNP mtandao linalojishugulisha na kupinga ukatiki wa kijinsia,Lilian Liund alisema kuwa lengo la kuandaa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari ni kujenga na kuongeza uelewa na uwezo wa waandishi wa habari kuripoti masuala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi.
Takwimu zinaonyesh hadi januari 2019 wanawake wakuu wa Nchi walikuwa 10 kati ya 152 ambapo wanawake wa wakuu wa serikali walikuwa 10 kati ya 193 kwa upande wa Afrika kwa sasa kumekuwa na Marais wawili wanawake,aliyekuwa Rais Maritius na Rais kutoka Etheopia aliyechaguliwa Okotoba 2018 na mawaziri wakuu mmoja kutoka Namibia aliongeza kusema Liundi.
Liundi alimaliza kwa kusema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa hadi januari 2019 kidunia masipika Mabunge ni 197 na manaibu sipika wanawake ni asilimia 28.2 kulingana na ripoti hiyo hiyo wabunge wanawake katika nchi zote walikuwa 24.3 pia kufikia june 2017 nchi zilizo kusini mwajangwa la Sahara kulikuwa na wastani wa wabunge wanawake 23.7.
Ilitufikie uchumi wa kati wa viwanda nilazima wanawake washirikishwe katika kukuza Tanzania kuwa katika kukuza uhumi wa kati hiyo nikuwajali wanawake na vijana ili kujenga uchumi tusiwachwe jinsia hata makundi mbali mbali tuungane wote pamoja katika kushiriki kwa namna gani kila moja ama nyingine kuhakikisha Tanzania inajengwa na makundi yote na kufikia uchumi wa kati.
