Mzalendo aomba kukutana na Rais Magufuli


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

 Katika kuonekana kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa Rais Dkt John Magufuli, wananchi wazalendo wameendelea kujitokeza hasa baada ya kazi nzuri inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo mmoja Kati ya wananchi wazalendo, Bwa, Rashidi Kayumbo anasema Sasa ni mda mwafaka kwa Tanzania kujengwa katika misingi ya Uzalendo.

Anasema kama atapendezwa, Rais wa nchi Mh. Dkt John Magufuli, ampe nafasi ya kuonana nae uso kwa uso ili Kama mwananchi mzalendo aweze kutoa ushauri wake sambamba na kuishauri serikali katika shughuri za maendeleo.

Wakati wa mahojiano na Muungwana blog, Bw. Rashidi Kayumbo amesema kuwa, imefika wakati wa kumshukuru Mungu kwa kumpata Rais ambaye ni mzalendo na anatetea haki za wanyonge, hivyo kuomba ridhaa ya kumuomba Mh, Dkt John Magufuli, kumpa ridhaa ya kwenda kuonana ikulu, na yeye Kama mzalendo aweze kutoa mawazo yake ya kizalendo.

 "Nakuomba Mh. Rais Dkt John Pombe Magufuli anitunuku ya kufika ikulu kwa ajili ya kuzifikisha hoja zangu, lakini pia kwa Uzalendo wangu napenda kumhakikishia mhe. Rais Kuna hoja za msingi katika kuishauri serikali ni wakati huu wa Sasa na Mimi ninayo maeneo ya kuishauri serikali katika shughuli za maendeleo" amesema Kayumbo.

Amebainisha Baadhi ya Mambo aliyowahi kutoa ushauri "Mnamo mwaka 2013 Mimi militia ushauri kwa mwandishi juu ya uliyokuwa kero katika mzani wa Kihonda Morogoro, barua ya Wizara katika kuthamini mawazo yangu ni Na BA/307/540/02/15/2013"

"Mwaka 2014 nilipeleka maoni yangu  niliandika barua kwenda Wizara ya ujenzi nilitaka kufanya ziara na wataalamu katika Baadhi ya barabara za jiji la Dar es saalam kupunguza msongamano wa mahari barua Na AS/MRS/CO/VOL/38/2014 ya tarehe 12/08/2014" alisema Kayumbo.

Pia ameomba serikali kuitambua sekta ya ugavi kwa makampuni ya ujenzi alisema sekta hiyo endapo itatambuliwa na kuhakikisha kila mtu anayefanya kazi hizo kuwa na TIN namba na EFD Mashine sekta hiyo unaweza kuongeza pato la Taifa kwa kulipa Kodi hivyo aliomba serikali iitambue sklekta hiyo.

"Ningependa uwepo ulazima wa kisheria kwa kila supplies kupatiwa mkataba wa mwandishi na kampuni au mkandarasi anayetaka kupewa huduma ya kupatiwa matilio kwa idadi na thamani halisi ya fedha na malipo yote yafanyike kupitia A/C za mabenki Kama kazi nyingine zilivyo" alisema.

 Amesema Mamlaka ya Mapato awe tayari kwanza kupikwa maelezo ya Supplies kulingana na gharama halisi za kazi Kisha serikali ipokee kiasi chake alisema endapo wazalendo Kama yeye watapata nafasi wanauwezo wa kukomesha vyanzo vya Mapato vilivyokuwa havijulikani na vikachangia pato la taifa.

 Amesema eneo Lingine analo shauri serikali kulifanyia kazi ni eneo la vibarua alisema vibarua wengi katika hii nchi wanalipwa isivyositahiki kwa maeneo mengi alisema kwa nijibu wa sheria kibarua anatakiwa kulipwa 12,500, lakini kundi hili Mara nyingi kumekuwa likilipwa elfu 5000,6000 Hadi elf 7000 kwa siku.

 Ameshauri ili kumaliza tatizo hilo ni serikali ianzishe mfumo wa makampuni na makandarasi wote kutumia fomu za kila siku na kwa kila kibarua ili kuona namna wanavyolipwa pia ameshauri kuwekwa siku ya wazalendo ili kujengwa mfumo wa kizalendo.