https://monetag.com/?ref_id=TTIb Serikali yataja vigezo vya kupandisha bei ya maji | Muungwana BLOG

Serikali yataja vigezo vya kupandisha bei ya maji


Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa, ameziagiza mamlaka za maji nchini kuongeza udhibiti wa maji yanayopotea, kabla ya kuongeza gharama za matumizi kwa watu.

Waziri Mbarawa amesema hayo wakati akizindua mradi wa maji katika Kijiji cha Shilima wilayani Kwimba, mkoani Mwanza ambao umejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza.

“Kuanzia sasa tutaweka utaratibu, kila mamlaka itatakiwa kufikisha wateja kiasi fulani, la sivyo itazuiwa kuongeza gharama kwa wateja wake” amesema Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na maombi mengi ya kuongeza gharama za matumizi ya maji, na kupelekea mamlaka nyingi kuingiza gharama hizo kwa wananchi kupitia ankara zao za malipo ya matumizi ya maji.