Simon Msuva ampeleka mdogo wake kutibiwa Morocco


Mshambuliaji wa timu ya Difaa El Jadid ya nchini Morocco na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Simon Msuva ameamua kumpeleka mdogo wake James Msuva nchini Morocco kwa ajili ya matibabu zaidi.

 James Msuva amekuwa na tatizo la nyama za paja, ambalo humuweka nje ya uwanja mara kadhaa na kushindwa kuwa na muendelezo mzuri uwanjani.

Saimon Msuva ambaye anaishi na kucheza soka la kulipwa nchini Morocco katika klabu ya Difaa El Jadid, aliamua kumuombea ruhusu mdogo wake katika klabu yake ya KMC kwa ajili ya kuondoka nae kwa gharama zake binafsi na kwenda kumpatia matibabu kwa madaktari wabobezi nchini Morocco.