Baraka Messa, Songwe.
Kuimarika kwa usimamizi mzuri watumishi wa sekta ya elimu, walimu kujituma na kuboreshwa kwa miundo mbinu mashuleni kwa ongeza kiwango cha ufaulu na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaomaliza shulebila kujua kusoma darasa la saba mkoani Songwe.
Afisa elimu mkoa wa Songwe Juma Kaponda amesama hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa wakati wa kukabidhi madawati kwa halmashauri nne za mkoa wa Songwe yaliyotolewa na ofisi ya mkoa wa Songwe.
Alisema mkoa wa Songwe mwaka huu kwa wanafunzi ambao wamemaliza darasa la saba kuwa ni wanafunzi watatu (3) tu wamebainika kuhitimu bil kujua kusoma tofauti na miaka mitatu ya nyuma ambapo mkoa huo ndipo ulianzishwa rasmi na kuwa na rundo la wanafunzi wanaohitimu darasa la saba bila kujua kusoma.
“matokeo yamekuwa yakibadilika kila mwaka hii ni kutokana na usimamizi mzuri wa viongozi, walimu kujituma katika kufundisha na miundo mbinu mizuri ambayo huwarahisishia wanafunzi katika ujifunzaji na walimu katika ufundishaji” alisema Kaponda .
Matokeo ya darasa la saba msimu wa 2017 mkoa wa Songwe ulikuwa na wastani wa 63 wa ufaulu ukishika nafasi ya 23 kitaifa, msimu wa 2018 mkoa ulikuwa na wastani wa kufaulu wa asilimia 74 na kushika nafasi ya 17 kitaifa na kuongeza kuwa mwaka huu mkoa unategemea kufikisha asilimia 80 kwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba juzi.
Aliongeza kuwa mkoa unaendelea na jitihada za kuboresha elimukwa kuboresha miundo mbinu ya madarasa, vyoo, madawati na kuhakikisha shule zote za msingi na sekondari kuhakikisha zinatoa chakula cha mchana mashuleni.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Songwe jeneral mstaafu Brigedia Nicodemas Mwangela alisema miongoni mwa sababu ambazo zinapelekea mkoa kutofanya vizuri kwenye sekta ya elimu kuwa nipamoja na walimu walimu kukosa uaminifu kwa kutofika kwa muda mwafaka katika vituo vyao vya kazi lakini pia kuwahi kuondoka wakati bado vipindi vya kufundisha vikiwa vinaendelea.
“ kuna baadhi ya walimu wanafika tu nakusaini kitabu cha mahudhurio alafu wanaondoka bila kufanya kazi ambayo ndio taaluma yao , afisa elimu kwa wale wakuu wa shule ambao hawawajibiki wote badilisha hatuwezi kuwa na nchi ya viwanda kama hatutoi wasomi wazuri “alisema mkuu wa mkoa
“Sehemu zingine idara zingine watumishi hawalali kutokana na kufanya kazi , wakurugenzi wa halmashauri zote fwatilieni mwenendo wa elimu kwenye maeneo yenu ili kuongeza ufaulu na kuboresha elimu ndani ya mkoa wetu ambao bado haufanyi vizuri sana.” Aliongez Mwangela.
Aidha Mkuu wa mkoa alizitaka Halmashauri zote za mkoa wa Songwe kukamilisha mapema ujenzi wa miundo mbinu ya madarasa na madawati na kudai kuwa kwa halmashauri ambayo itashindwa kukamilisha kufika mwezi novemba kuwa watumishi wake hawatapata mapumnziko ya mwishoni mwa mwaka .