Waandamanaji wanaopigania demokrasia Hong Kong wamekusanyika nje ya ubalozi mdogo wa Uingereza mjini humo, wakiitaka nchi hiyo iongeze juhudi kuwalinda wananchi wa koloni lake hilo la zamani na kuongeza shinikizo dhidi ya ukandamizaji wa uhuru unaofanywa na China.
Mamia ya waandamanaji waliimba wimbo wa taifa wa Uingereza, "God Save the Queen" na wimbo wa Kizalendo wa Uingereza ''Rule Britannia" nje ya ubalozi huo mdogo wa Uingereza, huku wakipeperusha bendera za Uingereza na bendera zilizotumika wakati wa ukoloni mjini Hong Kong.
Maandamano hayo makubwa yamefanyika tena leo kwenye mitaa ya Hong Kong na kuikiuka marufuku iliyowekwa na polisi ambayo ilionya kuwa mikusanyiko yote ni kinyume cha sheria.
Waandamanaji hao wanailaumu Uingereza kwa kutochukua hatua za kutosha kuikabili China kutokana na kuubinya uhuru wa ndani wa Hong Kong.