Na Thabit Madai,Zanzibar.
WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar, Khamis Juma Mwalimu amesema waandishi wa habari nchini wanawajibu mkubwa wa kuielimisha jamii juu ya uwepo na kazi za Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar kwa lengo la kufanya kazi kwa Mashirikiano.
Amesema jamii haina uwelewa wa kutosha kuhusu Tume ya kurekebisha sheria na kupelekea kukwamisha baadhi ya utendaji kazi wa tume hiyo kutokana kukosa mashirikiano na Jamii.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akifungua mkutano wa siku Moja kwa waandishi wa habari ulioandaliwa na Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar ambapo Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Shirika la bima Mpirani Mjini Magharib Unguja.
Waziri Khamis Juma alisema baadhi ya wananchi hawafahamu kwa kina juu ya uwepo wa Tume ya kurekebiha sheria na kazi zake licha ya kuwa Tume hiyo ipo kwa muda mrefu na inafanya kazi kwa mujibu wa Sheria.
Aliongeza kusema kuwa waandishi wa habari ndio wenye wajibu mkubwa wa kuelimisha jamii juu ya uwepo wa Tume hiyo na kazi zake.
“Waandishi wa habari ni kioo cha jamii hivyo ni vyema kutumia nafasi yao kuwaelimisha jamii juu ya uwepo, wajibu na kazi za tume hiyo kwa lengo la kufahamu na ushirikiana na tume hiyo wakati wa kurekebisha sheria mbali mbali” alisema Waziri.
Alieleza kuwa kufanya hivyo kwa waandishi wa habari kutasaidia wa kiasi kikubwa kuongeza uelewa wa wananchi na pindi watakapo shirikishwa katika kuchangia juu ya mabadilik mbali mbali ya sheria watakuwa na muamko wa kutoa maoni yao.
Katika hatua nyingine Waziri huyo aliwataka watendaji wa Tume hiyo kuongeza bidii na utekelezaji wa kazi za tume hiyo kwa lengo la kufankisha matarajio Nchi na Wananchi kwa Ujumla.
“Kiukweli Tume hii imebeba matarajio makubwa kwa Nchi na wananchi hivyo niwashauri kuwa wangeza biii katika utekelezaji wao wa kazi za sheria”alisema Waziri huyo.
Nae Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakari amesema lengo la Mkutano huo kwa wana habari ni kuwaelimisha waandishi wa habari wajue,kazi,wajibu wa tume kiundani.
“Tumeamua kuwaita nyinyi waandishi wa Habar wa vyombo mbali mbali ili uwaelisha kwa kina juu utendaji kazi wa Tume ya kurekebisha sheria na mujue nafasi yenu mwisho muelimishe jamii juu ya kazi za tume hiii”Alisema Jaji Mshibe.
Katika maelezo yake Jaji Mshibe alifahamisha kuwa lengo la tume hiyo kuona kuwa jamii inapata taarifa sahihi za sheria.
Kwa Upande wake Dkt Abuubakari Rajabu akiwasilisha mada kwa waandishi hao juu ya Wajibu wa waandishi wa Habari katika kuongeza ufahamu wa shughuli za kisheria, Dkt Abuubakari alisema kuwa waandishi wa habari wananjukumu la kutoa taarifa sahihi kwa jamii na wakati muafaka.
Alisema kuwa ni wajibu wa waandishi wa habari kutoa taarifa kwa jamii na kuwaelimisha jamii juu ya kazi na matukio mbali mbali yanayotokea Nchini.

