Na Thabit Madai,Zanzibar
Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi imepokea msaada wa miamvuli 27 kutoka kwa kampuni ya Bopaar Interprises kwa ajili ya kutumika katika kituo cha Daladala cha kijangwani kwa abiria wanaosubiri huduma za usafiri.
Akipokea miamvuli hiyo Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amesema miamvuli hiyo itatumika kwa muda wakati ujenzi wa vipanda vya kukalia abiria vikiendelea kujengwa.
Amesema kutokana na mazingira yalipo sasa kwenye kituo hicho ambapo kumekuwa na malalmiko ya abiria kukosa sehemu ya kujifichia jua wakati wakisubiria daladala,serikali ya Mkoa huo imetafuta miamvuli hiyo huku jitihada za kukamilisha vibanda hivyo zikiendelea.
“Baada ya kuiona chanagamoto hii ya kutokukamilika kwa vibanda vya kupumzikia abiaria tukaamua kutafuta miamvuli hii kwa wenzetu wa kampuni ya Bopar ili tulipatie ufumbuzi wa dharura tatizo hili na matumaini yangu itasaidia kwa kiasi katika kipindi hiki kifupi ambacho tunasubiria kakamilika kwa ujenzi”alisema Ayoub.
Aidha Mhe. Ayoub amesema lengo la kuwekwa kwa miamvuli hiyo ni kwa ajili ya abiria ambao walikuwa wakilalamikia kuwepo kwa changamoto hiyo ya kwa kuwepo kwa jua wakati wanasubiri gari.
“Tunaebdelea na ujenzi wa vipanda vya kusubiria gari ambapo tunajenga mabanda matutu makubwa na kukamilika kwa ujenzi huo tutakuwa tumemaliza changamoto zote kusiana na kituo hiki maana miundombinu yote imekmilika ikiwemo vyoo na taa”alisema Ayoub
Katika hatua nyengine Mkuu wa Mkoa ameuagiza uongozi wa Baraza la Manispaa ya Mjini kushirikiana na jeshi la police kusimamia kituo hicho cha kijangwani ili kuweza kudhibiti daladala ambazo zimekuwa zikikiuka taratibu zilizowekwa .
“Kumejitokeza kwa baadhi ya gari za daladala zimekuwa zikikiuka taratibu zilizowekwa ambapo zinatakiwa kuingia katika kituo hiki lakini haziingii ndani ya kituo na badala yake wanakiuka ruti zao,sasa ipo haja ya kuwepo usimamizi wa kituo hiki kupitia askari wetu wa manispaa ili atakaebainika achukuliwe hatua”alisema Mkuu wa Mkoa.
Mapema akikabidhi miamvuli hiyo muwakilishi kutoka kampuni ya Bopar enterprises Saleh Taimour amesema uongozi wa kampuni hiyo umepokea wito wa serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi wa kuhitajika miamvuli kwa ajili ya matumizi ya kituo hicho.
Amesema kampuni yao imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na serikali ya Mkoa huo kwa ajili ya shughuli mbali mbali za maendeleo na kwamba wametoa msada huo ili kutatua tatizo hilo katika kituo hicho.
Mkurugenzi Manispaa ya Mjini Said Juma Ahmada ameshukuru kampuni ya Bopar Enterprises kwa msada walioutoa ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ilipo huku uongozi wa manispaa ukiwa katika hatua za mwisho za kuimarisha miundombinu kituoni hapo.
“Tumepokea msaada huu wa miamvuli nishukuru uongozi wa Mkoa kwa miongozo unayotupa kuona kituo hiki kinafanya kazi kama ilivyokusudiwa na tunaondoa changamoto zilipo kwa haraka iwezekanavyo ili wanachi wetu waweze kupatiwa huduma ya usafiri bila matatizo yoyote lakini pia kwa sasa tutaweka askari wetu wa manispaa kama tulivyotakiwa waweze kusimamia na kuongoza na kuelekeza matumizi sahihi ya kituo hiki”alisema Said.