Waliohitimu mafunzo ya JKT waonywa wasitumike vibaya



Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Vijana waliohitimu mafunzo kwa mujibu wa sheria  wameonywa wasitumike na kutumiwa na watu wasio litakia mema taifa.


Onyo hilo limetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango kwa vijana hao waliohitimu mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria kupitia operesheni makao makuu Dodoma katika Kikosi cha Jeshi namba 843 kilichopo katika wilaya ya Nachingwea.

Muwango ambae alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Lindi katika mafunzo hayo, alisema vijana hao 1002 waliohitimu mafunzo hawanabudi kujiepusha kutumika na kutumiwa vibaya na watu wasio litakia mema taifa letu kupitia mafunzo waliyopata.

Alisema mafunzo waliyopata ni kwa maslahi ya taifa. Kwahiyo waishi kwamujibu wa viapo walivyoapa.

'' Viapo vyenu vinawataka muwe waaminifu, watiifu na wazalendo kwa taifa. Kwahiyo msikubali, mtateseka',, alionya Muwango.

Alibainisha kwamba vitendo viovu kama matumizi ya dawa zakulevya waviepuke ili waweze kutimiza ndoto za mafanikio katika maisha yao.


Aidha alitoa wito kwa wazazi na walezi wawaruhusu na kuwahamasisha watoto wao wajiunge na Jeshi la Kujenga Taifa kwani mafunzo yanayotolewa yanania nia njema kwao na taifa.

Kwaupande wake kamanda wa kikosi hicho (KJ 843)  Luteni kanali Nyagalu Malecela alisema vijana walioripoti kwa ajili ya mafunzo hayo ya kipindi cha miezi mitatu walikuwa 1042.

Hata hivyo waliohitimu ni 1002, huku vijana 40 wakishindwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali.Ikiwemo utoro, nidhamu na afya.

Malecela alisema muingiliano wa mafunzo na udahili wa wanafunzi wanaotaka kujiunga na kwa masomo ya elimu ya juu ni miongoni mwa changamoto katika mafunzo kwa vijana wanaochukua mafunzo kwa mujibu wa sheria.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items