Kamati maalumu yaundwa kuchunguza uzembe ajali ya moto Morogoro



Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema serikali imeunda kamati maalumu kubaini waliofanya uzembe baada ya ajali ya Moto iliyotokea mjini Morogoro na kusababisha vifo zaidi ya watu Mia moja.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akiahirisha shughuli za bunge, ambapo amesema tayari serikali imeunda kamati maalumu ili kuchunguza wale wote waliofanya uzembe au kushindwa kutekeleza majukumu yao na kupeleka kusababisha vifo kwa watanzania zaidi ya Mia moja.

"Ili kuwabaini wale wote ambao hawakutekeleza majukumu yao vizuri na kupeleka kutokea kwa maafa makubwa kwa watanzania, hivyo tumeunda kamati maalumu ambayo itachunguza na hatimaye kuwachukulia hatua kali wale wote waliozembea wakati wa tukio hilo" amesema Mhe. Waziri Majaliwa.

Aidha amewataka Tanzania kujifunza kutokana na tukio hilo hivyo matukio Kama hayo yasijitokeze tena kwa sababu yanapunguza nguvu kazi ya taifa.

Pia amesema katika vikao vya bunge vilivyokuwa kwa takribani wiki mbili na jumla ya maswali 123 yaliulizwa na maswali ya nyongeza 217, na maswali 6 ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu na jumla ya Muswada 4 na maazimio 8 yalipitishwa.

Ameipongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuwa mwenyekiti wa SADC, na kutoa hotuba nzuri iliyojaa matumain, na kupitisha kiswahili kuwa lugha rasmi ya Jumuiya hiyo na kwamba kutaongeza hali ya uwekezaji hapa nchini.

Pia ameitaka Wizara ya Kilimo kwenda kusimamia mawakala waliopewa kazi ya kusambaza pembe jeo za kilimo kwa wakulima na kuhakikisha pembejeo hizo zinafika kwa wakulima kwa wakati.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items