Afrika Kusini yazima ndoto za Japan kufikia nusu fainali Kombe la Dunia la Rugby


Afrika Kusini jana ilizima ndoto za Japan za kufikia nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa kuibamiza kwa 26-3 katika hatua ya robo fainali huko Tokyo na kujikatia tiketi ya kupambana na wakali Wales katika nusu fainali ya kombe la dunia la raga.

Japan iliitambia Afrika Kusini kwa 34-32 katika kombe la dunia lililopita lakini mechi ya jana iliyochezwa Tokyo ilikuwa zamu yao kulipiza kisasi mabingwa hao mara mbili duniani wa raga.

Afrika Kusini sasa imetinga nusu fainali na itacheza na Wales walioishinda Ufaransa kwa 20-19 mapema jana. Springboks ya Afrika Kusini iliyowahi kushinda Kombe la Webb Ellis mwaka 1995 na 2007, sasa ina ndoto ya kulinyakua kombe la dunia la 2019.