Austria: Kijana awaua wazazi wa mchumba wake


Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 25 amewapiga risasi watu watano na kuwaua hapo hapo jana  asubuhi huko Kitzbuhel, mji mdogo wa Alpine mashariki mwa Innsbruck, nchini Austria, kabla ya kujisalimisha kwa Polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi waliouliwa ni mpenzi wake wa zamani mwenye umri wa miaka 19 na kaka yake, wazazi na mchumba wake mpya. Eneo la uhalifu lilikuwa kama sinema.

Mshukiwa huyo, aliyetambuliwa kama Andreas E, alijitokeza katika kituo cha polisi na kukiri kwamba alikuwa amewauwa watu watano.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia