Msanii wa Hip-Hop nchini, Ibrahim Mussa maarufu kama Roma ni mfano halisi kuwa ndoa za mastaa kumbe zinawaweza kudumu kama za raia wa kawaida.
Jana rapper huyo na mke wake, Nancy wanasherehekea miaka minne ya ndoa yao na wanaendelea kuonesha kuwa thabiti.
Miaka minne iliyopita, walifunga ndoa yao. Wawili hao walifahamiana chuoni na kuwa na uhusiano kwa miaka mingine kibao kabla ya kufunga ndoa.
Roma ameshare picha kadhaa za ndoa yao kupitia ukurasa wake wa Instagram kuadhimisha siku hiyo.
Roma aliandika;
Tarehe Na Siku Kama ya Leo (jana), Miaka Minne Iliyopita, Nilifunga Ndoa Takatifu Na Pisi Flani Inaitwa NANCY
Mungu Ametubariki Vitu Vingi Saaaana Lakini Vikubwa Alivyotubariki Ni Hivi Hapa Vitano.
1.Tuko Hai Hadi Leo
2.Hatujaachana Wala Hatukuwahi Kuachana.
3. Mtoto wa kwanza Wa kiume IVAN.
4.Mtoto Wa Pili Wa Kike IVY.
5.HATUTAACHANA NG'OO.
#Happy4thAnniversary To Us.
