Changamoto za ndoa husababisha msongo wa mawazo


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella  Manyanya, amesema watanzania wengi wanachangamoto za kindoa hali inayosababisha msongo wa mawazo, mdororo wa kiuchumi na jamii isiyo na malezi bora.

Amesema kuwa asilimia 90 ya ndoa hizo zimekufa na wenza wake wanaishi kwa maonyesho na dhana ya kuvumiliana wakiona aibu kutengana hivyo ipo haja kufanyika kwa tafiti na kuwekeza nguvu katika elimu ya ndoa.

Hayo aliyasema  wakati akizindua Kitabu cha Siri za mafanikio ya Ndoa kilichoandaliwa na mtunzi ambaye ni Mchungaji na Mkurugenzi wa Fedha  wa Bohari ya Dawa (MSD), Dk. Sako Mayrick.

Naibu Waziri huyo alisema  Watanzania wengi wanachangamoto za kindoa hali inayosababisha msongo wa mawazo, mdororo wa kiuchumi na jamii isiyo na malezi bora.

“Ni kawaida watu kufanya sherehe za ndoa na kutumia gharama kubwa lakini ndoa zinazoishi na hai ni chache huku nyingi kuvunjika  kwake ni kimyakimya kwa dhana ya kuona aibu,”alisema.

Alisema changamoto hizo ndio zinazochangia ongezeko la wagonjwa wa akili,  baadhi ya watu kuwa na msongo wa mawazo uliopitiliza hadi kupasuka mishipa ya fahamu, gharama kubwa ikitumika kusafirisha baadhi ya wagonjwa nje ya nchi huku kiini cha matatizo ikiwemo ni migogoro iliyokithiri ya kifamilia.

“Imefika wakati wasomi wetu kutumia uwezo wao katika kutoa elimu ya ndoa na familia, na kujua  ndoa si fasheni tu, vitabu vya aina hii vinasahaulika hivyo iwe chachu ya  kupambana na matatizo yaliyopo kwakuwa vita ya uimarishaji wa ndoa katika jamii  inahitaji watu wa kiroho na kitaalamu wakiwemu wa ustawi ya jamii kushirikiana,” alisema.

Alisema utunzi wa vitabu hivyo pia ni fursa ya kuufikia uchumi wa kati wa viwanda hivyo  alimpongeza Sako kuandika kitabu hicho alichosema kitaisadia kurejesha amani na upendo kwa watu wengi hususani vijana kutokana na mafunzo yaliyomo.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items