China yakosoa hatua ya Marekani ya vikwazo dhidi ya makampuni yake

China imeitaka Washington kuondoa vikwazo vyake vipya dhidi ya kampuni za tekenolojia za China.

 Wizara ya mambo ya kigeni ya China kupitia msemaji wake Geng Shuang imekosoa vikali hatua ya karibuni ya Marekani ya kuyaingiza kwenye orodha mbaya makampuni makubwa ya kijasusi ya taifa hilo kwa kusema ni uingiliaji kwenye masuala ya ndani ya China.

Hata hivyo China haikusema iwapo itajibu hatua hizo. Kwa upande mwingine wizara ya biashara ya China imesema ujumbe wa mazungumzo ya kumaliza vita vya kibiashara na Marekani unaoongozwa na makamu waziri mkuu Liu He utaenda Washington tayari kwa majadiliano siku ya Alhamisi licha ya mzozo huu unaoibua wasiwasi.