Na Thabit Madai, Zanzibar
Mkuu wa wilaya ya Kaskazini “B” Unguja Rajab Ali Rajab amewewaomba wakulima wa zao la mwani Unguja kuwawastahamilivu kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wakati serikali iko mbioni kuzitatuwa changamoto hizo.
Wito huo ameutowa huko kiwengwa alipofika kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wa kulima wa mwani wa kijiji hicho.
Alisema afisi yake inafahamiu changamotowanazokabiliana nazo wakulima wa mwani na serikali kuu tayari imeshapanga mipango madhubuti ya kutatuwa changamoto hizo ikwemo mpango maalum wa kujengwa kiwanda cha kuchakata mwani.
Alisema shughuli ya ukulima wa mwani ni ngumu na iwapo ukilimwa na kuuzwa bila ya kufanywa kitu chochote inadhihirisha wazi kuwa wakulima hawapati faida, lakini kama utatengenezewa vitu hapa zanzizbar hata bei na thamani yake itapanda na wakulima wataweza kujikimu kupitia gharama za uzalishaji.
Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya alisema kabla ya ugatuzi wakulima wa mwani walikuwa wakipata baadhi ya misaada na baadhi ya vifaa kuuziwa kwa bei nafu, lakini tangu kufanywa kwa ugatuzi wamekuwa wakikosa fursa hiyo.
kutokana na hali hiyo aliwataka maafisa husika kurudisha utaratibu wa kuwasaidia wakulima wa mwani kwa taratibu watakazokubaliana baina ya halmashauri na idara ya maendeleo ya uvuvi.
Nao wakulima wa mwani wa kijiji cha kiwengwa wakizitaja changamoto hizo wamesema ni ukosefu wa vitendea kazi ikwemo kamba na vijiti pamoja na bei ndogo ya kuuza mwani wao.
Pamoja na changamoto hizo za mwani lakini pia wamsema wanakabiliwa na suala la uvuvi haramu ambapo wameiomba serikali iwasaidie kuondosha uvuvi huo unaofanywa na watu kutoka nje ya kiwengwa pamoja na ukosefu wa maji katika eneo la cairo.
Akizungumzia kuhusu kuporomoka kwa maadili kwa vijana wa kiwengwa mku huyo wa wialaya amewata wakaazi wa kijiji hicho kujitahmini wenyewe ,kwani wengi wamwekuwa wakiwakodisha vyumba watu wanaofanya baishara zisizofaa na baadae wanawalalamikia.
Alisema anazotaarifa ya kuwa chumba kimoja kinakodishwa zaidi ya watu watano na wanaokodi kwa ajilai ya kujistiri tu baada ya kufanya biashara zao zisizoweleweka.
Hata hivyo aliahidi katika kusaidi kuondioka kwa tabia chafu na mporomoko wa maadili katika kijiji hicho kwa kusaidiana na kamati ya ulinzi nausalama atarejea tena kufanya msako wa kukabilina na vitendo hivyo aliouita kwa jina la opereshen kiwengwa.
