DC Dodoma akagua mashine za EFD


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amefanya ziara kwenye maeneo ya Biashara jijini humo kukagua mashine za ulipaji kodi (EFD) pamoja na vitambulisho vya wajasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo.

Katika ziara hiyo DC Katambi ameongozana na Kamati ya Ushauri wa Kodi ya Wilaya ambapo walizunguka kwenye sehemu za Biashara kwa ajili ya kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa wafanyabiashara hao.

DC Katambi amewataka wananchi na wafanyabiashara Kwa ujumla kushirikiana na Serikali katika kuwabaini wale wote wanaokwepa kodi.